Star Tv

Miaka saba iliyopita Amol Yadav alitangaza kwa familia yake na marafiki kuwa angejenga ndege kwenye paa la nyumba yao katika mji wa Mumbai India.

Familia na marafiki waliokua wamepigwa na butwa walimuuliza rubani huyo ni vipi angeweza kuishukisha ndege ikikamilika . Walijikakamua kupandisha vifaa vya kuijengea ndege hiyo hadi paa la nyumba ya familia la ghorofa tano, ikiwemo injini iliyonunuliwa kutoka ng'ambo ya zaidi ya kilo 180.

Mwezi Februari mwaka uliopita, ndege hiyo ya injini moja yenye nafasi ya watu 6 ilikuwa imekamilika.

Kulingana na Bwa Yadavm, ndege hiyo ndiyo ya kwanza kujengewa nyumbani nchini India.

Anasema kuwa injini hiyo ina nguvu za kuiwezesha ndege hiyo kupaa umbali wa futi 13,000 na tanki lake linaweza kubeba mafuta ya kuiwezesha ndege hiyo kusafiri umbali wa kilomita 2000 kwa kasi ya kilomita 342 kwa saa.

Bwana Yadav sasa anasema kuwa yuko tayari kujenga ndege ya kwanza kabisa kujengwa India.

Wawekezaji wameonyesha moyo wa kuwekeza na serikali ya BJP imeahidi kumpa ekari 157 za ardhi za kujenga kiwanda cha kuunda ndege za kubeba abiria 19.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.