Star Tv

Watu 176 wamepoteza maisha baada ya ndege ya abiria ya Ukraine kuanguka na kuteketea moto viungani mwa mji mkuu wa Iran, Tehran.

Msemaji wa Shirika la Usafiri wa Anga la Iran Reza Jafarzadeh, amesema  waliofariki dunia katika ajali hiyo ya alfajiri ya leo Jumatano katika eneo la Parand kaunti ya Robat Karim mkoani Tehran ni raia wa Iran.

Jafarzadeh amesema abiria wote 167 na wahudumu tisa wameaga dunia katika ajali hiyo, na kwamba ndege hiyo ilikuwa ikielekea katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev.

Ali Khashani ambaye ni afisa wa ngazi za juu wa idara ya uhusiano mwema katika Uwanja wa Kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran amesema, ndege hiyo aina ya Boeing 737 ya shirika la kimataifa la ndege la Ukraine UIA imeanguka muda mfupi baada ya kupaa angani kutoka uwanja huo, na kuteketea moto.

Kwa mujibu wa afisa huyo amesema huenda ajali hiyo imesababishwa na hitilafu za kiufundi lakini akasisitiza kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kubaini kiini  cha ajali hiyo.

Afisa huyo wa Idara ya Uhusiano Mwema katika uwanja wa kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran ameongeza kuwa ajali hiyo haijatatiza ratiba na safari zingine za ndege.

                                                                                             Mwisho.

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.