Star Tv

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametishia kumchukulia hatua za kijeshi mbabe wa kivita nchini Libya, Khalifa Haftar, wakati akizungumza na wabunge wa chama  chake ikiwa ataendelea kuishambulia serikali ya mjini Tripoli inayotambuliwa kimataifa.

Haya yamejiri baada ya Haftar kuondoka katika mkutano wa upatanishi mjini Moscow hapo jana, bila kusaini makubalino ya kusitisha mapigano, ambayo kiongozi wa serikali ya mjini Tripoli ameyaridhia.

Rais Erdogan amesema atashiriki katika mkutano mwingine kuhusu amani nchini Libya, ambao utafanyika Jumapili ijayo mjini Berlin, Ujerumani, ukizishirikisha pia nchi za Ufaransa, Uingereza na Italia, na mataifa ya kiarabu kama Misri, Algeria na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Aidha, Uturuki imepeleka vikosi nchini Libya kuiimarisha serikali ya waziri mkuu Fayez al-Sarraj, na Rais Erdogan amesema vitabaki huko mpaka utulivu utakapopatikana nchini humo.

                                                                                               Mwisho.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.