Star Tv

Baraza la Seneti la Marekani limemuondolea hatia Rais Donald Trump na kuhitimisha mchakato wa mashtaka dhidi yake, ambapo wabunge wa chama cha Democratic walimtuhumu kutumia vibaya madaraka yake.

Wanachama wa chama cha Democrats walimshtaki Rais Trump mnamo mwezi Disemba na kushinikiza Ukraine kumtia mbaroni mpinzani wa White House.

Warepublican walio wengi katika baraza hilo walipata kura 52 ya kumuondoa hatiani Trump, dhidi ya kura  48 za upande uliounga mkono kumtimua katika wadhifa wake.

Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na Kidemokrasia liliidhinisha nakala za mashtaka mnamo tarehe 18 Disemba.

Katika kura yake ya kihistoria Jumatano, Seneti iliamua kutomuondoa rais wa 45 wa Marekani madarakani kwa mashtaka yanayotokana na kushughulika kwake na Ukraine.

Wanachama wa chama cha democratic walihitaji theluthi mbili ya kura katika baraza hilo lenye wajumbe 100, ili kuweza kumtia hatia Rais Trump.

Kiongozi wa maseneta wa chama cha Democratic Chuck Schumer ameipuuza kura hiyo iliyomtakasa Trump akisema haina maana yoyote, kwa sababu Walipublican walikataa katakata kusikiliza mashahidi.

Rais Trump alikuwa akishutumia  kwa kuomba msaada kwa serikali ya Ukraine kumsaidia achaguliwe tena mwezi Novemba,kusitisha kutoa misaada ya mamilioni ya fedha pamoja na msaada wa kijeshi kwa Ukraine mpaka rais wa nchi hiyo afanye uchunguzi dhidi mpinzani wake.

Aidha, hatua kadhaa zilipitiwa ili madai hayo kuitwa kesi ambapo  mnamo Agosti 2019 watu walitoa madai dhidi ya rais Trump, Oktoba – Disemba uchunguzi ulifanyika , licha ya chama cha Trump kuwa na viti vingi zaidi ya wapinzani wake, mwezi Disemba kiongozi wa Democratic alipiga kura kumshtaki rais Trump na mwezi Januari 2020: Kesi ilifikishwa kwa seneti.

                                                                                              Mwisho.

 

Latest News

WAKRISTO KUJITAFARI NA KWARESMA.
26 Feb 2020 17:45 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padre Dokta Charles Kitima amesema kipindi cha kwaresima ni fursa ya kuji [ ... ]

CORONA YAENDELEA KUONGEZA IDADI YA VIFO IRAN.
26 Feb 2020 10:58 - Grace Melleor

Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa  [ ... ]

BURIANI RAIS HOSNI MUBARAK.
26 Feb 2020 10:00 - Grace Melleor

Aliyekuwa rais wa zamani nchini Misri ambaye alitawala taifa hilo kwa miaka 30 Hosni Mubarak amefariki dunia hapo jana F [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.