Star Tv

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amemshutumu Rais Donald Trump, kwa kuleta mgawanyiko na kutumia vibaya mamlaka yake.

Katika maoni aliyoyatoa Bwana Mattis amesema rais Trump ameamua kugawanya watu wa Marekani na pia ameshindwa kuonesha uongozi uliokomaa.

Anasema alikasirishwa na kufadhaishwa sana na jinsi Bwana Trump alivyoshughulikia maandamano ya hivi karibuni.

Tangu wakati huo amekuwa kimya hadi utawala wa Trump ulipokosolewa vikali katika gazeti la Atlanta Jumatano.

Bwana Mattis aliandika katika gazeti la The Atlantic..“Donald Trump ndio rais wa kwanza kwa maisha yangu ambaye hawaunganishi raia wa Marekani "Badala yake, anajitahidi kutugawanya, Tunashuhudia miaka mitatu ya hatua hizi za kukusudiwa na tunashuhudia matokeo ya miaka mitatu ya uongozi ambao haujakomaa.

Bwana Mattis pia alizungumzia wimbi la hivi sasa la maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi ambako kuchochewa na kifo cha raia Mmarekani mweusi George Floyd aliyekufa mikononi mwa polisi mapema mwezi huu.

Bwana Mattis alijiuzulu 2018 baada ya rais kuamua kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Syria.

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.