Star Tv

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa Florence Parly ametangaza kifo cha kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abdelmalek Droukdel aliyekuwa nchini Mali na "wasaidizi wake kadhaa", wakati wa operesheni ya kijeshi iliyofanyika Juni 3 nchini Mali.

Operesheni iliyoendeshwa Juni 3 Kaskazini mwa Mali na vikosi vya Ufaransa kwa msaada wa washirika wao ilisababisha kifo cha kiongozi (Amir) wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Aqmi Abdelmalek Droukdel.

Waziri wa Jeshi Florence Parly wa Ufaransa alitangaza Ijumaa Juni 5 kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa kiongozi wa kundi hilo tayari ameuawa.

Operesheni hiyo ilitekelezwa Kaskazini mwa eneo la Adrar des Ifoghas, kilomita 80 Mashariki mwa Tessalit, karibu na mpaka na Algeria.

Habari hii ilikuwa bado haijathibitishwa kwa sababu shambulizi hilo dhidi ya kiongozi huyo lilitekelezwa na ndege isiyokuwa na rubani ya jeshi la anga la Ufaransa, likifuatiwa na mashambulizi ya helikopta.

Ndipo ilipotolewa taarifa na waziri wa Jeshi wa Ufaransa kuwa watu 5 , kiongozi wa kundi la Aqmi Abdelmalek Droukdel na wasaidizi wake, ikiwa ni pamoja na afisa mwandamizi anayehusika hususani na propaganda katika kundi la Aqmi waliuawa katika mashambulizi hayo.

"Vikosi vya Ufaransa vilivyotumwa katika operesheni vinathibitisha kwamba leo jkiongozi wa kijihadi Abdelmalek Droukdel ameangamizwa"  amebaini Kanali Frédéric Barbry, msemaji wa makao makuu ya majeshi ya Ufaransa, na kuongeza kuwa wameweza kumamata mmoja wa wapiganaji hao, Huku ikiarifiwa kuwa mmoja wa wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi alijisalimisha bila kupigana.

Abdelmalek Droukdel ni kiongozi wa kijihadi katika ukanda huo, na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kwenye makundi kadhaa ya jihadi katika ukanda wa Sahel, pamoja na kundi la JNIM au GSIM kwa Kifaransa, kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu.

Kulingana na chanzo rasmi, vipimo vya damu vilivanywa na kubaini kwamba mmoja kati ya watu waliouawa ni Abdelmalek Droukdel.

Mwishoni mwa mwaka wa 2018, jeshi la Ufaransa lilitangaza kifo cha Amadou Koufa, kiongozi wa kundi la katiba Macina, kabla ya mtu huyo kuonekana tena kwenye video miezi michache baadaye.

Ufaransa kwa sasa inasubiri kuona iwapo kundi hilo la Aqmi litatangaza kifo cha kiongozi wao.

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.