Star Tv

Mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden amemtaja Seneta Kamala Harris kama mgombea mwenza-akiwa ni mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kugombea wadhifa huo.

Bi. Harris ambaye wakati mmoja alikua hasimu wake katika mchuano wa kuwania urais, ni seneta wa California mwenye asili ya India-na Jamaica ambaye kwa muda mrefu amekua akichukuliwa kama mgombea wa nafasi ya pili baada ya Biden.

Mwanasheria huyo mkuu wa zamani wa California amekua akitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi katika polisi ya Marekani wakati wa maandamano ya kitaifa ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Bi Harris anasema wakati wote amekuwa akijivunia utambulisho wake na anajieleza binafsi kama ''Mmarekani".

Mwaka 2019, Bwana Biden aliliambia jarida la Washington Post kwamba wanasiasa hawapaswi kupewa nafasi kisa tu ya rangi au wanakotoka.

Katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House Jumanne, Bwana Trump ambaye ni Mrepuplican alimuelezea Bi Harris kama '' Mtu ambaye wa kwanza ninayeweza kumchukua''

Bi Harris atakua na mjadahalo na mgombea mwenza wa Trump, Makamu wa rais Mike Pence, tarehe 7 Oktoba Salt Lake City, Utah.

Aidha, ni wanawake wengine wawili tu ambao wamewahi kugombea viti vya Makamu wa Rais nchini Marekani ambao ni Sarah Palin kutoka chama cha Republican mwaka 2008 na Geraldine Ferraro wa Democrats mwaka 1984, hata hivyo hakuna mmoja wao aliyeweza kufika White House.

Bwana Joe Biden anatarajia kukakabiliana na Rais Donald Trump katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 3 Novemba mwaka huu.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.