Star Tv

Wanafunzi 10 wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya bweni la shule yao ya Byamungu English Medium Primary School iliyoko wilayani Kyerwa mkoani Kagera kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 14,2020.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesitisha shughuli za malazi katika shule hiyo kwa mud na ameelekeza kamati za usalama za ngazi zote katika mkoa wa Kagera kufanya mapitio upya ya shule zinazotoa malazi, kuhakiki kwamba shule hizo kama zinavyo vibali halali vya serikali na ubora wa majengo yanayotumiwa na wanafunzi, na kuangalia mifumo ya uzimaji moto na kujiokoa inapotokea ajali ya moto.

Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni hilo, na mpaka sasa chanzo cha moto bado hakijajulikana.

Matukio ya shule kuungua moto yamekuwa yakitokea mara kwa mara ambapo mapema mwezi Julai, wanafunzi watatu wa shule ya sekondari ya Ilala Islamic walipoteza maisha baada ya shule yao hiyo iliyo jijini Dar es Salaam kuungua moto, Mwezi wa nane shule ya St.Joseph Sekondari iliyopo jijini Mwanza bweni liliungua moto.

 

Latest News

HESLB YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA POTOFU INAYOSAMBAZWA MITANDAONI.
19 Oct 2020 17:32 - Grace Melleor

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefafanua kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na utara [ ... ]

WAALIMU WAANZA MGOMO DR CONGO.
19 Oct 2020 17:02 - Grace Melleor

Nchini DRC, walimu kutoka chama cha walimu cha SYECO na wale kutoka chama cha walimu wa kikatolika (SYNECAT) wameanza mg [ ... ]

WANANCHI WA GUINEA WASUBIRI MATOKEO YA UCHAGUZI WA URAIS.
19 Oct 2020 16:25 - Grace Melleor

Baada ya miezi kadhaa ya maandamano mabaya dhidi ya muhula wa 3 wa rais Alpha Condé, wananchi wa Guinea walipiga kura k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.