Star Tv

Mkuu wa polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema waliohusika na ajali ya moto iliyowaua watoto 10 wa shule ya msingi Byamungu Islamic iliyoko wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Kamanda Sirro wakati akizungumza na Waandishi wa Habari amebainisha kuwa shule hiyo ilikuwa na hitilafu nyingi zikiwemo namna ambavyo wayaringi ya jengo hilo imefanyika pamoja na matofali yaliyotumika kujengea shule hayakuwa imara.

''Kikubwa Hatujafahamu chanzo hasa ni nini, lakini kwa haraka inaonekana jengo halikuwa madhubuti, ndio maana tumemkamata mwenye shule. Lakini pia nimesema wamtafute Afisa Elimu na Wakaguzi wote waliokuwa wanakuja kukagua hii shule, walikuwa wanaona watoto wanakaa wapi?, jengo lilikuwa imara?, ni lazima hapa tuwe wakali kwasababu tayri maisha ya watu yamekwisha ondoka''-Amesema Kamanda Sirro.

Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni wakati ajali ya moto ilipotokea ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Aidha, Kamanda Sirro amesema kuwa wanajaribu kutafuta vyanzo ikiwa ni pamoja na uwezekano wa adui wa nje kutumia mwanya kufanya jambo hilo, amewataka wakazi wa Kyerwa kushirikiana kutoa taarifa zozote juu ya chanzo cha ajali hiyo.

Latest News

HESLB YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA POTOFU INAYOSAMBAZWA MITANDAONI.
19 Oct 2020 17:32 - Grace Melleor

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefafanua kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na utara [ ... ]

WAALIMU WAANZA MGOMO DR CONGO.
19 Oct 2020 17:02 - Grace Melleor

Nchini DRC, walimu kutoka chama cha walimu cha SYECO na wale kutoka chama cha walimu wa kikatolika (SYNECAT) wameanza mg [ ... ]

WANANCHI WA GUINEA WASUBIRI MATOKEO YA UCHAGUZI WA URAIS.
19 Oct 2020 16:25 - Grace Melleor

Baada ya miezi kadhaa ya maandamano mabaya dhidi ya muhula wa 3 wa rais Alpha Condé, wananchi wa Guinea walipiga kura k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.