Star Tv

Mkuu wa Wilaya ya kahama Anna Mringi Macha amepiga marufuku biashara ya nyama ya nguruwe na usafirishaji wa nguruwe wenyewe baada ya wanyama hao kubainika kwa homa ya nguruwe.

Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu huyo wa wilaya alisema amechukua uamuzi huo ili kukinga wananchi na watumiaji wa nyama hiyo dhidi ya ugonjwa huo.

“Maeneo yanayofanya biashara ya nyama ya nguruwe, vichinjio, wapishi na sehemu za starehe haziruhusiwi kufanya biashara hiyo kwa sasa mpaka itakapotangazwa tena”-Macha alisema.

Bwana Macha alisema dalili za mlipuko wa ugonjwa huo zilianza Desemba mwaka jana na sasa ni kama unasambaa.

Bwana Macha pia alipiga marufuku usafirishaji wa wanyama hao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali cha daktari na atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Daktari wa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dkt. Damian Kilyenyi amethibitisha kuwa zaidi ya nguruwe 500 wamekufa kwasababu ya ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Wataalamu wa afya Homa ya Nguruwe ni ugonjwa wa kupumua unaosababishwa na virusi ya influenza aina A, vinavyofahamika kama H1N1, Chanzo chake ni kwenye nguruwe, lakini sasa huambukiza binadamu na huenezwa kwa kupiga chafya au kukohoa.

Dalili za ugonjwa huo zinakaribiana na za homa ya msimu ambayo dalili zake ni kupata homa kali, kukohoa, maumivu kooni, maumivu mwilini na mzizimo, Na wanaoathirika zaidi huwa ni wajawazito, watoto wa chini ya miaka mitano, wazee wa zaidi ya miaka 65 na wale wenye matatizo mengine ya kiafya.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.