Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinachoitwa Mwanza Precious Metals Refinery (MPMR).

Kiwanda hiki kilichozinduliwa na Rais Samia kimetajwa kuwa kikubwa zaidi kuliko vyote Afrika Mashariki na kazi yake kubwa itakuwa kusafisha dhahabu za kimataifa, Ambacho kwa siku moja kiwanda hicho kina uwezo wa kusafisha dhahabu kilo 480.

Kiwanda hicho ambacho kimegharimu thamani ya Bilioni 12.2 za Kitanzania sawa na dola za Kimarekani Milioni 5.2 katika uwekezaji wake kitasafisha dhahabu yote ya Tanzania

Aidha aliongeza kusema kuwa jukumu la serikali sasa ni kuweka sera, sheria ambazo zitawawezesha wachimbaji wachimbe zaidi malighafi ipatikane kwa wingi zaidi.

Mwanza Precious Metals Refinery ni miongoni mwa viwanda vitatu vipya vilivyoanzishwa nchini, Ambapo kwa sasa dhahabu za ndani ya nchi hazitasafirisha tena kwenda nje ya nchi.

Aidha, ukamilishwaji wa kiwanda cha MPMR ni ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Madini la Taifa STAMICO yenye asilimia 25 na kampuni za Rozella General Trading LLC ya Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na Kampuni ya ACME Consultant Engineers PTE Ltd ya Singapore zina ubia wa asilimia 75.

Kuanza rasmi kwa usafishaji wa Dhahabu katika kiwanda cha Mwanza Precious Metals Refinery (MPMR) ni matokeo ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini kuendelea Kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kusafisha, kuchenjua na kuongeza thamani kufanyika ndani ya nchi hiyo.

Rais Samia amesema Benki kuu sasa itaweza kununua dhahabu katika kiwanda cha MPMR kwa mujibu wa sheria.

"Mtambo huu utawezesha Benki Kuu ya Tanzania BOT yetu kuanza kununua dhahabu kwa mujibu wa sheria na hivyo kuwezesha nchi yetu kuwa na amana ya dhahabu yaani Tanzania sasa tutaanza kuwa na gold reserve kwenye BOT yetu".-Rais Samia.

Mtendaji mkuu wa kiwanda hicho, Anand Mohan ameishukuru Serikali kwa kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho huku akisema kitachangia kukuza uchumi wa Tanzania.

Aidha katika upande mwingine Rais amezinfua jingo la ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na kutaka Benki hiyo kusimamia na kuweka mikakati ya kuhamasisha benki ndogo kutoa mikopo ya muda mrefu kwa wananchi na kuweka riba nafuu ikiwa ni pamoja na kutondoa masharti magumu kwa wakoji.

“Viwango vikubwa vya riba visiwe vikwazo kwa wananchi kukopa, nipenda viwango vilivyopo vishushwe kama nilivyoelekeza angala u kwa 10% kwenda chini ili kuwawezehsa Watanzania kuweza kukopa”-Alisema Rais Samia.

Pia Rais ametaka marekebisho yafanyike katika kutoza kodi, Ambapo amebainisha kuwa VAT kwa madini yanayoletwa kutoka nje idaiwe baada ya kuchenjua.

Uzinduzi wa kiwanda hiki ambacho ni miongoni mwa vikubwa zaidi barani Afrika kutaifanya Tanzania kuuza nje madini ambayo yamekwishachakatwa.

Kwa sasa Tanzania inaungana na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda na Rwanda kuwa na viwanda vya kuchakatia dhahabu zake.

 

Latest News

NIGERIA YAPOKEA NDEGE SITA ZA KUPAMBANA NA WAASI.
23 Jul 2021 14:50 - Grace Melleor

Nigeria imepokea ndege sita za kijeshi iliyonunua kutoka Marekani, ambazo zinatarajiwa kupiga jeki juhudi za kukabiliana [ ... ]

WATU KADHAA WAKAMATWA KWA JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA RAIS RAJOELINA.
22 Jul 2021 13:15 - Grace Melleor

Raia kadhaa wa mataifa ya kigeni pamoja na wengine wa nchini Madagascar wanashikiliwa na mamlaka nchini humo kwa tuhuma  [ ... ]

HABARI ZA HIVI PUNDE: ANNA MGHWIRA AFARIKI DUNIA.
22 Jul 2021 10:55 - Grace Melleor

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Julai 22, katika Hospitali ya Mount Meru.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.