Star Tv

Watanzania wanaozungukwa na bonde la Mto Kihansi ambalo ni maarufu kwa uwepo wa vyura adimu duniani wanajulikana kama ‘Chura waKihansi’ wameombwa kushiriki utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira wametoa wito huo kwenye zira ya kujifunza kujifunza shughuli mbalimbali za uhifadhi wa vyanzo vya maji katika bonde hilo na kutaka elimu zaidi itolewe juu ya faida mbalimbali za bonde hilo mkoani Morogoro.

Mbunge wa Moshi Vijijini ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo Anthony Komu, amesema eneo la bonde la Kihansi ni kubwa lakini ni eneo dogo tu lililohifadhiwa hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kufanya kilimo kinachoharibu vyanzo vya maji.

Naye, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Bi. Hawa Mwaifunga amesema, ziara hiyo imemuongezea uelewa na umuhimu wa kuhifadhi mazingira na utunzaji vyanzo vya maji kwani kabla alikuwa anasikia tu kama hadithi.

Awali akitoa historia ya bonde hilo lenye utajiri wa viumbehai adimu, Mratibu wa mradi huo Bi. Amina Kibola amezishukuru taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo TAWIRI, vyuo vikuu vya SUA na UDSM kwa kushirkiana na Ofisi ya Makamu wa Rais kuhakikisha ustawi wa mradi wa Kihansi.

Kwa muda mrefu sasa NEMC imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali na wadau wengine kuhakikisha vyura wa kihansi ambao walikuwa hatarini kupotea kutokana na shughuli za kibinadamu wanakuwa salama na kurudi katika mazingira ya asili ya bonde hilo.

Picha na mtandao.

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.