Mfanyabiashara wa vyuma chakavu wilayani Serengeti mkoani Mara imembidi kujisalimisha kwa jeshi la polisi mjini humo baada ya kugundua kauziwa Bomu kwa shilling elfu nne kama chuma chakavu.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara wa vyuma chakavu mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara Jonas Marwa amejikuta katika wakati mgumu baada ya kugundua kauziwa Bomu kama chuma chakavu kwa shilling elfu nne. Baada ya kubaini kitu hicho kinacho shabihiana na bomu ndipo alipokwenda polisi kuomba msaada. Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huu imefika na kushuhudia bomu hilo huku wakikiagiza kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania 21 KJ kufika na kulitegua. Ununuzi wa vyuma chakavu katika maeneo mengi mkoani Mara ni moja ya vitu vinachotakiwa kuwekewa utaratibu maalumu kutokana na wanunuzi na waletaji wa bidhaa chakavu kutokuwa makini na kuokota vitu vinavyoweza kuleta madhara katika jamii.

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.