Changamoto ya mimba za utotoni umesababisha zaidi ya wanafunzi 1000 wamekatisha masomo mkoani Mwanza katika kipindi cha miaka mitatu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna amesema kuwa takwimu hizo ni zile zilizotolewa taarifa kwenye madawati ya jinsia ya polisi.

Kamanda wa polisi anasema kuwa takwimu hizo zinaashiria tatizo la mimba linaendelea kuathiri jamii hususan watoto wa kike. Mkurugenzi wa shirika la Kivulini Yasini Ally amesema kuwa changamoto kubwa ambayo inaikumba jamii kwa hivi sasa ipo kwenye malezi ya watoto na kusababisha baadhi ya watoto kujitumbukiza kwenye mahusiano yasiyo salama.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha kuweka mikakati wa namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa waathirika wa vitendo vya ukatili mkoani Mwanza wametoa rai kwa wadau kushirikiana
Wadau kikao hicho kimewashirikisha waandishi wa habari,madaktari, polisi na maafisa maendeleo ya jamii kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa mwanza.

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.