Star Tv

NEC imesema inatumia fedha za ndani katika zoezi la maboresho ya Daftari la kudumu la wapiga kura ili kuifanya Tume hiyo kuwa huru na kuwajibika bila kuingiliwa na wahisani katika mipango na mchakato wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Wakati Tanzania ikitarajiwa kuingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la wapiga kura zoezi ambalo litaanza Julai mwaka huu. Dkt. Athumani Kihamia Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ametolea
ufafanuzi wa wapiga kura watakaokutwa na zoezi la uchaguzi wakiwa eneo tofauti na walipojiandikisha na kwamba Tume hiyo ipo tayari kuwaruhusu kupiga kura kama kutafanyika marekebisho ya sheria ya sasa ya uchaguzi. Hata hivyo suala la ushiriki wa watu wenye ulemavu bado limeonekana kutotiliwa mkazo huku walemavu wakilalamikia miundombinu isiyo rafiki inayowanyima haki ya kupiga kura. Maamuzi yoyote katika mchakato wa uchaguzi mara nyingi huwagusa kwa kiasi kikubwa wanawake ambao mara nyingi hujiandikisha kwa wingi na kupiga kura tofauti na wanaume. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeendelea kukutana na wadau mbalimbali na kutoa elimu juu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura ambapo imekutana na Asasi za wanawake, Walemavu na Vijana.

Latest News

Kumbukumbu ya miaka 20 ya Hayati Mwalimu Nyerere
14 Oct 2019 12:52 - Kisali Shombe

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwa [ ... ]

Mgogoro machimbo ya Shilalo Mwanza: Serikali yasitisha uchimbaji wa Dhahabu
11 Oct 2019 10:14 - Grace Melleor

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani [ ... ]

Kesi Ya Uhujumu Uchumi: Sethi Na Rugemalira Waandika Kuomba Msamaha
11 Oct 2019 09:46 - Grace Melleor

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.