Star Tv

Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewatembelea majeruhi 43 wa ajali ya moto iliyotokea Agosti kumi mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuwapatia kila mmoja Shilingili 500,000 kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Ajali hiyo iliyotokea Jumamosi Agosti 10, 2019 katika mtaa wa Itigi, Msamvu mkoani Morogoro mita 200 kabla ya kufika kituo cha mabasi cha Msamvu barabara ya Morogoro- Dar es Salaam baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta. Rais Magufuli amewashukuru wauguzi pamoja na madaktari kwa huduma nzuri na kuwataka kuendelea na moyo huo huo wa kuwahudumia watanzania. Majeruhi 46 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro walihamishiwa Muhimbili, watatu kati yao wamefariki dunia. Rais Magufuli pia amewaagiza  madaktari kuhudumia majeruhi hao na kuwapatia mahitaji
yoyote wanayohitaji kwa gharama ya Serikali.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.