Star Tv

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara imekamata kilo tano za mchanga wenye madini ya dhahabu ukiwa na thamani ya shilling milllioni ishirini na tano ukitoroshwa kwenda kutafutiwa soko maeneo mengine.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa Mara Adam Malima ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi na wachimbaji madini toka katika mgodi wa Ilasanilo Buhemba kufuatia kuwepo kwa taarifa juu ya wao kukataa kujenga ukuta kwa lengo la kuzuia utoroshaji madini. Serikali haipo tayari kuona watu wachache wanakwamisha shughuli hiyo na kukosa mapato hivyo kama hawapo tayari mgodi huo utafungwa. Viongozi wa wachimbaji wadogo katika mgodi huo wanakili kuwepo kwa tatizo hilo huku wakisema ujenzi wa ukuta utasaidia kukabiliana na wimbi la wizi wa madini. Ni mwezi mmoja sasa tokea kufunguliwa kwa mgodi wa Ilasanilo Buhemba baada ya kufungwa kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya mashimo kudaiwa kuhatalisha maisha ya wachimbaji.

Latest News

ZANZIBAR YAFUNGUA MILANGO KWENYE UTALII.
06 Jun 2020 10:30 - Grace Melleor

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu kuanzia leo safari za ndege za kitalii kuwasili nchini baada ya mambukizi ya [ ... ]

UFARANSA YATANGAZA KIFO CHA KIONGOZI WA AL-QAEDA.
06 Jun 2020 08:27 - Grace Melleor

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa Florence Parly ametangaza kifo cha kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abde [ ... ]

MZOZO WA SERIKALI YA LIBYA NA HAFTARI WAENDELEA KUSHIKA KASI.
06 Jun 2020 07:20 - Grace Melleor

Serikali ya Libya yadai kuuteka mji muhimu kutoka kwa hasimu wake Khalifa Haftar.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.