Star Tv

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP Augustino Mrema ameitaka Serikali kumlipa Shilingi bilioni mbili kama fidia ya kesi alizowahi kushtakiwa chini ya serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa inaongozwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Mrema ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini dar es salaam wakati akizungumzia hali ya kisiasa nchini katika kipindi cha miaka 24 iliyopita hadi sasa.

Mwenyekiti huyo wa TLP amesema kutokana na misukosuko aliyoipata kwa kufunguliwa kesi za mara kwa mara, Serikali inapaswa kumlipa fidia ya kiasi hicho cha fedha.

 “Ninataka serikali ya CCM ambayo ndio imenufaika na mateso niliyopata kwa miaka yote wanifidie shilingi bilioni 2, hela ndogo ya chumvi na wasiponifidia nitawashtaki kwa watanzania.” Amesema Augustino Mrema-Mwenyekiti wa TLP Taifa.

Katika hatua nyingine Mrema amesema hakufurahishwa na vitendo vilivyofanywa katika uchaguzi wa serikali za mitaa hasa katika kijiji cha Kiraracha wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro akieleza kuwa zilikuwa ni hujuma za wazi dhidi yake.

Mbali na fidia, pia Mrema aliyepata kugombea nafasi ya Urais na kuleta upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995 amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli iliyo na malalamiko na kuomba kukutana naye ili waweze kuzungumza.

                                                                                                       Mwisho.

 

Latest News

WAZIRI UMMY ATHIBITISHA KUPONA KWA MGONJWA MMOJA WA COVID-19.
03 Apr 2020 15:58 - Grace Melleor

Waziri wa Afya nchini Ummy Mwalimu amesema kuwa mgonjwa mwingine aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) [ ... ]

TANZANIA YAPATA NEEMA TENA KUTOKA BENKI YA DUNIA.
03 Apr 2020 07:18 - Grace Melleor

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari , Dokta Hassan Abbas amesema tayari serikali imepokea Dola Mili [ ... ]

RAIS MUSEVENI ATANGAZA SIKU 14 KWA RAIA WAKE KUKAA NDANI YA MAKAZI YAO.
31 Mar 2020 10:30 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.