Star Tv

Naibu wa  Waziri wa Ardhi Nyumba na  maendeleo ya Makazi  Angelina Mabula amesema wakulima  wanapaswa kupimiwa maeneo yao ili kutokemeza migogoro ya ardhi nchini kwakuwa wataweza kujipatia hati miliki  ya ardhi zao.

 Naibu waziri  huyo amebainisha hayo  wakati akikabidhi hati miliki za kimila mia moja kwa  wakulima wadogowadogo  katika kijiji cha Litowa  Mkoani Ruvuma ambazo zimetolewa na mtandao wa wakulima Mviwata kwa kushirikiana na Halmsahuri ya Wilaya ya Songea.

 Mabula amesema hati hizo za kimila zilizotolewa zimelenga kutokemeza migogoro ya ardhi pamoja na kuongeza uzalishaji wenye tija

Kwa upande wake Mratibu wa MVIWATA Mkoa wa Ruvuma Laika Haji amesema utoaji wa hati hizo miliki umelenga kulinda usalama wa  ardhi huku Mwenyekiti wa kijiji hicho  Fabiani Shawa akiamini utolewaji wa hati hizo miliki utasaidia kukuza kilimo na kupunguza migogoro ya ardhi ambayo inapoteza muda wa wakulima kuisulisha.

Zaidi ya hati za Kimila 1700 zimetolewa katika Mkoa wa Ruvuma katika wilaya za tunduru, Madaba na Songea Vijijini ambapo  zaidi ya wananchi 1700 tayari wananufaika na urasimishaji huo wa ardhi.

 

                                                                                         Mwisho.

Latest News

DAWA ZA KULEVYA ZASHIKILIWA ZIKISAFIRISHWA KWA MFUMO MPYA.
21 Feb 2020 18:10 - Grace Melleor

Polisi Mkoani Morogoro wamegundua mfumo mpya unaotumika kusafirisha  madawa ya kulevya kwa njia ya pikipiki na tayari w [ ... ]

KESI YA UCHOCHEZI YA TUNDU LISSU YAENDELEA KUPIGWA KALENDA.
21 Feb 2020 17:50 - Grace Melleor

Upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu umeomba muda [ ... ]

MAJANGA YALIYOKUWA YAKIZIKUMBA NCHI ZA SADC SASA BASI.
21 Feb 2020 17:43 - Grace Melleor

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein amewataka mawaziri wanaoshiriki mkutano w [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.