Star Tv

Tanzania imeutaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada za kuleta amani katika maeneo yenye migogoro Barani afrika hususani katika Nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuipunguzia Tanzania idadi kubwa ya wakimbizi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani amesema hayo katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 33 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Nchini Ethiopia.

Katika hatua nyingine Tanzania imeuahidi Umoja wa Afrika kuendeleza mapambano ya maradhi mbalimbali hatari ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango wa Umoja huo kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030.

Katika Mkutano huo pia kumeshuhudiwa mabadiliko katika nafasi ya uenyekiti ambapo Mwenyekiti anayemaliza muda wake na rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi ambaye mikoba yake ya Uenyekiti ameikadhi kwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini Mhe. Cyrill Ramaphosa ambae anakuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika.

                                                                                                      Mwisho.

 

Latest News

WAKRISTO KUJITAFARI NA KWARESMA.
26 Feb 2020 17:45 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padre Dokta Charles Kitima amesema kipindi cha kwaresima ni fursa ya kuji [ ... ]

CORONA YAENDELEA KUONGEZA IDADI YA VIFO IRAN.
26 Feb 2020 10:58 - Grace Melleor

Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa  [ ... ]

BURIANI RAIS HOSNI MUBARAK.
26 Feb 2020 10:00 - Grace Melleor

Aliyekuwa rais wa zamani nchini Misri ambaye alitawala taifa hilo kwa miaka 30 Hosni Mubarak amefariki dunia hapo jana F [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.