Star Tv

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara Yonna Keawo ametoa muda  wa miezi minne,  kuhakikisha  fedha zote zilitotengwa na halmashauri hiyo  kwa ajili ya kukamilisha  baadhi ya miradi ya maendeleo iliyoanzishwa  kwa nguvu za wananchi,  zinapelekwa kwenye miradi hiyo.

Taarifa na  Zacharia Mtigandi

Baadhi ya miradi hasa ya sekta ya  afya katika halmashauri ya mji wa Babati iliyoanzishwa na wananchi wakitegemea kupata fedha za umaliziaji kutoka halmashauri ya mji huo  haijakamilika.

Kutokukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati  ni hoja mojawapo iliyoibuliwa na madiwani katika  kikao chao cha  baraza.

Hoja hiyo imemsukuma mwenyekiti wa halmashauri ya mji Yonna Keawo kuagiza fedha za bajeti zilizotengwa zitumike kukamilisha miradi hiyo ndani ya miezi minne kuazia sasa.

Hoja zingine zilizoibuliwa kwenye kikao hicho cha baraza la madiwani halmshauri ya mji wa Babati ni kuhusu shule ya msingi Daraji ambayo iko hatarini kutokana na kushambuliwa na wadudu aina  mchwa ambayo inahitaji kufanyiwa marekebisho.

Hata hivyo kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Babati Elizaberti Kitundu amesema ofisi yake tayari imetenga zaidi ya shilingi laki sita kusaidia ukarabati wa shule hiyo ya msingi Darajani.

                                                                        Mwisho.

Latest News

WAKRISTO KUJITAFARI NA KWARESMA.
26 Feb 2020 17:45 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padre Dokta Charles Kitima amesema kipindi cha kwaresima ni fursa ya kuji [ ... ]

CORONA YAENDELEA KUONGEZA IDADI YA VIFO IRAN.
26 Feb 2020 10:58 - Grace Melleor

Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa  [ ... ]

BURIANI RAIS HOSNI MUBARAK.
26 Feb 2020 10:00 - Grace Melleor

Aliyekuwa rais wa zamani nchini Misri ambaye alitawala taifa hilo kwa miaka 30 Hosni Mubarak amefariki dunia hapo jana F [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.