Star Tv

Serikali inaendelea kuchunguza kwa kina uwepo wa tishio la uvamizi  wa  Nzige  ambao wanadaiwa kuingia katika maeneo ya  Mwanga na Holili mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Taarifa na Zephania Renatus

Taarifa  zilizozagaa  kwenye mitandao ya kijamii na ambazo zimezua taharuki kwa watanzania ni  juu ya tishio la uvamizi wa  Nzige  ambao wanadaiwa kuingia katika badhi ya maeneo ya Wilaya ya  Mwanga karibu na nchi jirani ya Kenya.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira amezungumza na waandishi wa habari  na na kuwatoa wasiwasi watanzania kuwa nzige hao huenda walipita tu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa huo.

Taarifa hiyo inakuja huku baadhi ya wakazi wa maeneo ya Holili na Taveta  katika Mpaka wa Tanzania na Kenya  hawajaona nzige hao na bado wanaonekana katika baadhi ya maeneo ya nchi jirani ya Kenya.

Wakati hofu hiyo ikiendelea kutanda ,hata hivyo wakulima katika maeneo ya mpakan wanaomba serikali kuchukua tahadhari  kabla wadudu hao hawaingia nchini Tanzania.

                                                                       Mwisho

Latest News

WAKRISTO KUJITAFARI NA KWARESMA.
26 Feb 2020 17:45 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padre Dokta Charles Kitima amesema kipindi cha kwaresima ni fursa ya kuji [ ... ]

CORONA YAENDELEA KUONGEZA IDADI YA VIFO IRAN.
26 Feb 2020 10:58 - Grace Melleor

Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa  [ ... ]

BURIANI RAIS HOSNI MUBARAK.
26 Feb 2020 10:00 - Grace Melleor

Aliyekuwa rais wa zamani nchini Misri ambaye alitawala taifa hilo kwa miaka 30 Hosni Mubarak amefariki dunia hapo jana F [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.