Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ameitaka Ofisi ya CAG kufanya kazi kwa bidii na weledi pasipo kuogopa na kutishwa na awaye yeyote yule.

Rais Magufuli ametoa wito huo leo alhamisi Machi 26, 2020 wakati akikabidhiwa ripoti ya CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) na Bwana Charles Kichere pamoja na Ripoti ya TAKUKURU 2018/2019 kutoka kwa Brigedia Jenerali John Mbungo .

Kutokana na ripoti hiyo iliyosmwa leo na kukabidhiwa kwa Rais aliyekuwa ameandamana na Viongozi wengine wakiwemo Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Spika wa bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine imeonyesha upotevu wa hela zinazolipwa kama mishahara hewa kwa watu waliokufa.

“Serikali haiwezi lipa mishahara ya watu waliokufa kwa taasisi ya Polisi wakati pingu na Lockup mnazo nyinyi”-Rais Magufuli.

Aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema ni lazima uchaguzi Mkuu ufanyike mwaka huu licha ya janga hili lililopo la ugonjwa wa virusi vya Corona.

Katika ripoti hizo alizozipokea leo amesema zitaweza kufikishwa mapema bungeni ili kujadiliwa kwa lengo la kuzidi kukuza uchumi wa taifa hili.

Miongoni mwa ripoti zilizokabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais ni Ripoti ya Ukaguzi wa Serikali kuu, Ripoti ya Ukaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ripoti ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma, Ripoti ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo, Ripoti ya Ukaguzi wa Mifumo ya Tehama, Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi, Ripoti ya ufuatiliaji wa Mapendekezo yaliyotolewa katika Ripoti za Ukaguzi wa Ufanisi kwa Miaka iliyopita na Ripoti 12 za Ukaguzi wa Ufanisi katika Sekta mbalimbali ambazo ni


Kwa Mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 143 ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa 2005) kifungu kidogo 2 na 4 kinamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukabidhi Ripoti hizo kwa Mheshimiwa Rais kabla ya Tarehe 31 Machi kila mwaka na baada ya hapo ripoti hiyo inawasilishwa bungeni siku saba za mwanzo za kikao cha Bunge kinachofuata.
                          Mwisho.

Latest News

“HII CORONA IMETUWEKA KATIKA HALI NGUMU”-RAIS KENYATTA.
01 Jun 2020 14:21 - Grace Melleor

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la idadi ya watu walioambukuzwa virusi vya corona k [ ... ]

WAKILI AKIITA KIFO CHA GEORGE FLOYD MAUAJI YALIYOPANGWA.
01 Jun 2020 06:32 - Grace Melleor


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya  [ ... ]

MAANDAMANO YAENDELEA KUTANDA MAREKANI KUFUATIA KIFO CHA FLOYD.
30 May 2020 10:22 - Grace Melleor

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mau [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.