Star Tv

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tundu Lissu hii leo amezungumzia kuhusu hatari anayoiona mbele yake wakati huu akitarajia kurejea nchini Tanzania.

Lissu amesema hayo alipokuwa akizungumza na Watanzania kwa njia ya mtandao akiwa ughaibuni, kuhusu safari yake yakurudi nchini anayoitarajia hivi karibuni na wasiwasi alionao kuhusu usalama wake.

''Wale waliokuja kuniua hiyo siku ya tarehe saba Septemba miaka mitatu iliyopita na waliowatuma au waliowalipa au waliowaelekeza bado wanaitwa watu wasiojulikana, maana yake ni kwamba hao watu bado wapo na kwa sababu bado wapo na hawajasema kama lengo lao la kuniua wameliacha, bado kuna hatari juu ya maisha yangu.Kwa hiyo ninarudi nchini kwangu katika mazingira ambayo hatari dhidi yangu haijaondoka bado. Lakini ninarudi tu, ni nyumbani kwetu, inabidi nirudi,"-amesema Lissu.

Kwa mujibu wa Lissu, katika miezi sita iliyopita, uongozi chini ya Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe aliandika barua mbili kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania, ili kuomba apatiwe ulinzi atakaporudi.

Amesema hadi sasa anasubiri majibu ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao ndio wenye jukumu la kuhakikisha kuwa yuko salama atakaporejea nchini humo.

"Naomba niseme hili kwa ajili ya kumbukumbu, mimi sina na siwezi kuwa na jeshi binafsi la kunilinda, sina na siwezi kuwa na rafiki au taasisi au nchi, ''Hata kutujibu barua tu kusema kuwa tumepokea barua yenu tunaifikiria, hawajafanya hivyo."

Lissu anatarajiwa kurejea Julai 28 akiwa mmoja wa wanaoomba kuteuliwa na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Latest News

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

WASIOLIPA KODI KUFUNGIWA NAMBA ZA SIRI.
09 Jun 2021 08:46 - Grace Melleor

Mamlaka ya mapato nchini Kenya (KRA) inatarajiwa kuzifungia jumla ya nambari ya siri 66,269 za kulipa kodi ambazo hazitu [ ... ]

RAIS SAMIA AHUSIA WANAWAKE KUJIAMINI, MAITI KUTOZUIWA KUZIKWA.
08 Jun 2021 18:28 - Grace Melleor

Rais Samia Suluhu Hassani amewataka wanawake nchini kujenga utamaduni wa kujiamini kwakuwa ukombozi wa mwanamke unaanza  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.