Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza siku 07 za maombolezo ya kitaifa kuanzia Ijumaa ya leo Julai 24, kufuatia kifo cha rais mstaafu wa awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kilichotokea Dar es Salaam.

Rais amesema kuwa katika kipindi chote bendera zitapepea nusu mlingoti.

Aidha Rais Magufuli amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwa watulivu, wastahimilivu na wamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi cha kuondokewa na mpendwa wao rais Mstaafu Mkapa.

Rais huyo mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu amefariki akiwa na miaka 81.

Rais John Pombe Magufuli alitangaza usiku wa kuamkia leo Ijumaa kupitia runinga ya taifa taarifa za kufariki dunia kwa Mzee Mkapa katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

''Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu amefariki. Amefariki kwenye hospitali mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa. Niwaombe watanzania tulipokee hili. Taifa limepata msiba mkubwa. Tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki," alitangaza rais Magufuli.

Taarifa hiyo hata hivyo haikuweka wazi Rais Mkapa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani.

Katika ukurasa rasmi wa Rais Magufuli wa mtandao wa Twitter rais Magufuli amemuomboleza Mkapa na kusema atamkumbuka "kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa, ucha Mungu, uchapakazi na utendaji wake katika kujenga uchumi."

Rais Mkapa alizaliwa Novemba 1938, Mkoani Mtwara Kusini mwa Tanzania, na aliliongoza taifa hili la Tanzania kwa mihula miwili toka mwaka 1995 mpaka 2005.

Latest News

TANZANIA YATOBOA SIRI YA FURAHA YAKE CHINI YA UENYEKITI WA SADC.
13 Aug 2020 18:09 - Grace Melleor

Tanzania imejivunia mafanikio yaliyopatikana wakati ikiwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), c [ ... ]

MHADHIRI UDOM KIZIMBANI KWA RUSHWA YA NGONO.
13 Aug 2020 16:57 - Grace Melleor
Notice: Undefined property: stdClass::$thumb in /var/www/html/startv.co.tz/public_html/startvweb/modules/mod_minifrontpage/themes/default/tmpl/bottom.php on line 79

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma inatarajiwa kuwafikisha mahakamani watu 10 kat [ ... ]

OMBI ZITO KWA RAIS WA BURUNDI KUTOKA MUUNGANO WA WANAHABARI.
13 Aug 2020 14:45 - Grace Melleor

Muungano wa wanahabari nchini Burundi, umetoa wito kwa rais Évariste Ndayishimiye kuwasamehe wanahabari wanne wa Gazeti [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.