Star Tv

Bilionea Saniniu Laizer kutoka Mirerani mkoani Manyara, ambaye wiki kadhaa zilizopita mnamo mwezi Juni alipata Madini yenye uzito mkubwa zaidi kuwahi kutokea ambayo aliyauza kwa serikali na kuingia kwenye orodha ya mabilionea wapya wa Tanzania nyota yake imeendelea kung'aa.

Hatimaye Bilionea huyo leo ameuza jiwe lingine la Tanzanite kwa Serikali lenye kilo 6.3 na kukabidhiwa mfano wa hundi ya shillingi Bilioni 4.8.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo Agosti 03 Mirerani baadhi ya viongozi wa serikali waliweza kuhudhuria hafla hiyo ili kushuhudia makabidhiano hayo akiwemo Waziri wa Madini Dotto Biteko na Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango.

Kwa upande wake Bilionea Laizer ametoa wito wa kutokukata tamaa kwa wafanyabiashara na wachimbaji wengine wadogo wa madini, Ambapo amesema yeye binafsi alianza kuwa mfanyabiashara mdogo wa madini kwa miaka 10 na hajawahi kukata tamaa;
“Mimi nawashauri wachimbaji wadogo wasikate tamaa, mimi imenichukua miaka 10 katika shughuli hizi, nao ipo siku watafanikiwa”- Saniniu Laizer

Saniniu Kuryan Laizer mwenye umri wa miaka 52, ni mume wa wanawake wanne na amejaliwa watoto 30.

 

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.