Star Tv

Katika kuhakikisha kwamba tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo inaongezeka ili kujitosheleza kwa chakula na malighafi za viwandani, Wizara ya Kilimo imeendelea kuhamasisha matumizi ya mbolea ili kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta moja kama ilivyopendekezwa na wakuu wa nchi za Afrika kupitia Azimio la Abuja la mwaka 2006.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameeleza kuwa bei ya mbolea msimu wa 2020/21 imepungua kwa wastani wa shilingi 1,316 kwa mfuko wa kilo 50 wa UREA ikilinganishwa na msimu wa 2019/20, Na kwa upande wa DAP bei imepungua kwa wastani wa shilingi 2,860 kwa mfuko wa kilo 50 ikilinganishwa na msimu wa 2019/20.

Waziri Hasunga ameeleza hayo leo tarehe 11 Agosti 2020 ameyasema hayo wakati akitangaza bei mpya ya Mbolea kwa msimu wa mwaka 2020/2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Uingizaji wa mbolea kupitia BPS ambao unahusu mbolea za Urea, DAP, NPK, CAN na SA hivyo BPS umefanya gharama za usafirishaji wa mbolea baharini kushuka kwa kiasi kikubwa kutoka Tshs 23,000/= hadi Tshs 2,350/= Tshs kwa mfuko mmoja wa kilo 50.

Amesema kuwa pamoja na punguzo hilo la bei ya mbolea kwa msimu wa 2020/21 ukilinganisha na msimu wa 2019/20, vyama vya ushirika vilivyoshiriki zabuni ya BPS kwa msimu huu wa mwaka huu vitawauzia mbolea wanachama wao kwa bei nafuu zaidi ya bei elekezi inayotolewa na Serikali.

Waziri Hasunga amesema kuwa mbolea iliyoagizwa na vyama vya ushirika imewafikia wanachama wao mpaka vijijini walipo pasipo adha wala usumbufu wowote.

Aidha, kuhusu wastani wa bei ya mbolea ya DAP kitaifa kuanzia leo tarehe 11 Agosti 2020 kwa msimu wa 2020/21 itakuwa shilingi 55,573 kwa mfuko wa kilo 50 ikilinganishwa na shilingi 58,433 kwa mfuko wa kilo 50 msimu wa 2019/20.

Kwa upande wa mbolea ya UREA, wastani wa bei kitaifa kwa msimu wa 2020/21 itakuwa shilingi 48,070 kwa mfuko wa kilo 50 ikilinganishwa na shilingi 49,386 msimu wa 2019/20, huku waziri hasunga akifafanua mchanganuo wa bei elekezi za mbolea kutofautiana kimkoa ambapo amesema kuwa mbolea ya DAP na UREA kwa Mkoa mmoja na mwingine zinatofautiana kutokana na umbali kutoka Dar es Salaam, hali ya barabara na gharama za usafiri.

 

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.