Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ihakikishe Watanzania hawarubuniwi ili watumie vizuri utashi wao wa kisiasa kuchagua viongozi bora.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 12, 2020 alipofungua jengo la Intelijensia TAKUKURU Makao Makuu Dodoma. Amewasihi watumie vizuri ofisi hiyo kukusanya taarifa muhimu za kiintelijensia zinazowahusu wagombea, vyama au wananchi watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu.

“Sote tunatambua kuwa Oktoba, mwaka huu Taifa letu litaendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani… mna jukumu zito la kuhakikisha Watanzania hawarubuniwi na msimuonee au kumpendelea yeyote kwa maslahi yenu binafsi.”

Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 28, 2020 na kwamba wanawajibu wa kuchagua Serikali bora na kiongozi bora atakayewaletea maendelea maendeleo. “Chagueni kiongozi mwenye maono aliyetenda na atakayetenda.”

“Tayari tumeshuhudia mking’ata baadhi ya wagombea waliojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye hatua za awali za uteuzi wa wagombea kupitia vyama vyao. Msiache; endeleeni kukaza uzi na kuwadhibiti wote wenye kujihusisha na vitendo hivyo,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema wakati Taifa linapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, ni vyema Watanzania wote na viongozi wakazingatia nasaha za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika moja ya hotuba zake alipowataka wajiulize kwamba mgombea anayetumia rushwa kununua kura amepata wapi fedha hizo na je, akipata uongozi, fedha hizo atazirudishaje.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapongeza Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na watendaji wa TAKUKURU kwa kusimamia vema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ndani na nje ya Serikali.

 

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.