Star Tv

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma inatarajiwa kuwafikisha mahakamani watu 10 katika mahakama za Dodoma na Bahi na kuwafungulia mashauri yanayohusiana na Rushwa akiwemo Mhadhiri Msaidizi Chuo kikuu cha Dodoma akihusihwa na rushwa ya ngono.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 13,2020 jijini Dodoma, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo Sosthenes Kibwengo amesema kwa kushirikiana na ofisi ya taifa ya mashtaka, watamfikisha mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Bw.Jacob Paul Nyangusi [43]mhadhiri Msaidizi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Baada ya kumfikisha mahakamani, watamfungulia shauri la uhujumu uchumi kwa kosa la kutaka rushwa ya ngono kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11 /2007 ikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza na vifungu vya 57(1)na 60(2) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2020.

Bwana Kibwengo amefafanua kuwa,Majira ya saa 3 usiku wa tarehe 3,Oktoba,2018 TAKUKURU ilimkamata Bw.Nyangusi nyumbani kwake eneo la Nyumba Mia tatu jijini Dodoma muda mfupi kabla hajatekeleza nia yake ovu ya kufanya ngono na aliyekuwa mwanafunzi wake wa mwaka wa kwanza wa shahada ya sanaa katika jiografia na Mazingira.

Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoani Dodoma,ameendelea kufafanua kuwa ,awali TAKUKURU ilipokea taarifa kuwa mtuhumiwa alimtaka mwanafunzi wake huyo kingono kama sharti la kumsaidia ili aweze kufanya mitihani ya marudio na kumwezesha kufaulu katika somo lake ,na ndipo ikaweka mtego na kumkamata.

 

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.