Star Tv

Gavana wa Benki kuu Tanzania Florens Luoga amesema muda sio mrefu itaweka kanuni za kuhakikisha fedha zinazotokana na madini zinarudi Nchini kwani wawekezaji walikua wnadanganya kwa sababu ya kuwa na akaunti za benki nje ya nchi na kusababisha fedha kutorudi Nchini.

Taarifa na Salma Mrisho.

Akiwa Mkoani Geita kwa ziara ya siku moja na kutembelea mgodi wa dhahabu wa geita pamoja na maeneo mengine kuangalia hali ya uzalishaji wa dhahabu unavyofanyika.

Luoga  amesema kuwa haiwezekani Tanzania kuwa na dhahabu za kutosha halafu hakuna eneo la kuhifadhi dhahabu na kuongeza kuwa hivi karibuni kutakua na kanuni za uhifadhi wa dhahabu.

Uwepo wa masoko ya dhahabu umechangia kupatikana kwa mapato ambapo kuanzia machi 2019 hadi januari 2020 umeshazalisha tani tatu za Dhahabu zenye thamani ya bilioni 362.

Suala la kituo cha kuhifadhi dhahabu nalo limezungumzwa na kuonekana kama changamoto inayowakabili wawekezaji hao ambapo BOT wamesema  watakaa na kulifanyia kazi.

Halmashauri ya Mji wa Geita tayari imetenga maeneo ya kimkakati kwa shughuli mbalimbali za sekta ya madini.

                                                           Mwisho.

 

 

Add a comment

Basi la kampuni ya Premier linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mbeya limegongana uso kwa na lori lenye namba za usajili T486 ANU ambalo lilikuwa likivuta tela lenye namba T 775 APT na kusababisha vifo vya Watu wawili na majeruhi nane.

Ajali hiyo ambayo imehusisha basi na lori imetokea majira ya asubuhi  katika kijiji cha Inyala wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya.

Jitihada zilofanywa ni kuliondoa lori ambalo lilikuwa limeegeshwa barabarani ili kuruhusu magari mengine yaweze kupita na kuendelea na safari kwenye barabara hiyo pamoja na  kuwakimbiza majeruhi hospitali.

                                                                 Mwisho.

 

Add a comment

Leo tarehe 29/01 katika Bunge la 11 kikao cha pili, hati zilizowasilishwa mezani ni pamoja na taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2019 ambazo zitawasilishwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali. Vile vile uwasilishwaji wa taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa kuhusu usimamizi wa matumizi ya fedha za umma katika serikali za mitaa kwa mwaka 2019,ambazo zitawasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa.

Add a comment

Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni kitovu cha uhifadhi wa simba duniani kutokana na kuwa na wanyamapori hao wanaokadiriwa kufikia zaidi ya elfu kumi na saba ambao wamekuwa kivutio kikumbwa kwa wageni wanaoingia nchini kujionea rasilimali hiyo muhimu katika hifadhi za taifa.

Taarifa na Sadick Hunga…….

Add a comment

Bunge la 11 mkutano wa 18 limeanza leo tarehe 28/1/2020, bunge hili ni mahususi kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za mwaka za kamati za kudumu za Bunge., ambapo Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Na. 5), wa mwaka 2019, na muswada wa sheria ya ususluhishi wa mwaka 2020.

Add a comment

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza maombolezo ya kitaifa baada ya kufariki Rais wa pili wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi.

Add a comment

Wanafunzi zaidi ya 2700 wa shule ya msingi Bangulo iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam wanalazimika kutumia matundu ya vyoo nane tu hali inayotajwa kuwapa shida wanafunzi hao wakati wanapohitaji kujisaidia huku shule hiyo ikiwa na jumla la madarasa 14 pekee ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi  shuleni hapo

Habari na Adam Damian.

Add a comment

Rais Dokta John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi mbalimbali leo Februari 03,2020 ambao  aliwateua hivi karibuni.

Add a comment

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo na hali za watanzania wanaoishi jimboni Wuhan nchini China kwa ujumla kutokana na kuzuka kwa virusi vya homa ya Corona nchini humo.

Habari na Angela Mathayo.

Add a comment

Latest News

MIKE POMPEO: CHINA NA URUSI ZINAFICHA TAARIFA ZA CORONA.
26 Mar 2020 10:23 - Grace Melleor

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amedai kuwa serikali za Urusi na China zinajiepusha kutoa taarifa sahihi  [ ... ]

RAIS MAGUFULI:OFISI YA CAG FANYENI KAZI MSITISHWE.
26 Mar 2020 10:04 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ameitaka Ofisi ya CAG kufanya kazi kwa bidii na weledi pasip [ ... ]

WAZIRI WA ULINZI SUDAN AFARIKI DUNIA.
25 Mar 2020 10:24 - Grace Melleor

Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Luteni Jenerali Jamaleldin Omar, amefariki  kufuatia mshtuko wa moyo akiwa Sudan Kusini waka [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.